RIPOTI YA UZINDUZI WA KIKAO CHA KWANZA CHA BODI

Chama cha Wachimbaji Madini Wanawake Tanzania (TAWOMA) kilianzishwa tarehe 22mwezi August, mwaka 1997 na kusajiliwa rasmi tarehe 23 Novemba mwaka 1997 na kupatahati ya usajili namba 9280. Lengo la kuanzishwa kwake ilikuwa ni kuhamasisha wanawakewengi kuingia kwenye Sekta ya Madini na kuwakomboa kiuchumi kupitia Elimu, Mitaji naMasoko. Chama kilianza na wanachama 22 mwaka 1997 na mpaka sasa tupo wanachamazaidi ya 2,000 katika mikoa yote Tanzania bara.Lengo kuu la uanzishwaji wa...

RIPOTI YA MKUTANO MKUU WA 24 MAZINGIRA BORA MIGODINI KWA MAENDELEO YA WANAWAKE NA UCHUMI WA TAIFA

Viongozi waandamizi wa TAWOMA wakiongozwa Mwenyekiti wa chama, Bi. Gilly Rajah na Katibu, Bi. Salma Ernest walimuongoza mgeni rasmi Mhe. Waziri Dkt. Doto Biteko kutembelea mabanda ya maonyesho na kushuhudia utaalamu, huduma, bunifu mbalimbali kutoka kwa wadau wa sekta ya madini. Mabanda yaliyotembelewa ni pamoja na TAWOMA Vijana, TAWOMA Shop na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO). Katika maonyesho hayo, Mhe. Waziri alipata pia wasaa wa kusikia changamoto mbalimbali zinazowakabili...