IBRAHIMU SHINENI

Naitwa Wakili Ibrahim Shineni. Ni wakili mwandamizi nafanya kazi na law firm
inayofahamika kama LAW DOMAIN ADVOCATES iko mtaa wa Lumumba na
mkunguni Dar es salaam.
Nafanya kazi za kisheria na za ushauri kuhusiana na mambo ya biashara, taasisi
mbalimbali za kijamii zinazojiendesha bila faida na zinazojenga ustawi wa jamii
kwa kujitolea.
Nimekuwa mshauri na katibu wa makampuni mbalimbali nchini, ninauzoefu wa
kutoka wa uanzishaji na uendelezaji wa makampuni, mashiririka, taasisi
mbalimbali za kijamii na zile zisizo za kiserikali (NGO) kwa ujumla.
Nahudumu kama mjumbe wa bodi mbali mbali za makampuni, taasisi za
elimu na mashirika mbalimbali kwa muda na nyakati tofauti tofauti.