RIPOTI YA UZINDUZI WA KIKAO CHA KWANZA CHA BODI

Chama cha Wachimbaji Madini Wanawake Tanzania (TAWOMA) kilianzishwa tarehe 22
mwezi August, mwaka 1997 na kusajiliwa rasmi tarehe 23 Novemba mwaka 1997 na kupata
hati ya usajili namba 9280. Lengo la kuanzishwa kwake ilikuwa ni kuhamasisha wanawake
wengi kuingia kwenye Sekta ya Madini na kuwakomboa kiuchumi kupitia Elimu, Mitaji na
Masoko. Chama kilianza na wanachama 22 mwaka 1997 na mpaka sasa tupo wanachama
zaidi ya 2,000 katika mikoa yote Tanzania bara.
Lengo kuu la uanzishwaji wa chama ni kuwaendeleza na kuwawezesha wanawake walio
katika mnyororo wa thamani wa Madini na kwenye jamii zao katika kuainisha changamoto
zao, Kiuchumi, Mazingira ya kazi, Kifedha, Kitaalam, Kiteknolojia pamoja na Mahitaji yao
mengine Muhimu ili kuwakomboa na kuwaondoa kwenye Umasikini na kuongeza pato la
Taifa.

Free Exclusive Traffic Tips

About the Author: Secretary Tawoma

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *