UTAMBUZI WA MCHANGO WA MWANAMKE KATIKAMNYOROROWA THAMANI YAMADINIMIGODINI TANZANIA
Tanzania Women Miners Association (TAWOMA) ina zaidi ya wanachama elfu nne ambao
wanajishughulisha na shughuli za uchimbaji madini katika mikoa 21 na wilaya 41 Tanzania
Bara. Utafiti uliofanywa na Tanzania Women Miners Association (TAWOMA) kwa ufadhili wa
STAMICO ukihusisha sampuli ya wanawake wachimbaji madini 1000 katika mikoa ya
Shinyanga, Geita, Mara na Simiyu ulibaini changamoto mbalimbali ambazo wanawake
wachimbaji madini wanakabiliana nazo kwenye uchimbaji madini, umiliki wa migodi, usagaji
mawe na uchenjuaji, usafishaji, uongezaji thamani, upatikanaji wa mikopo na mitaji, na
ukosefuwa vifaa vya kisasa vya uchimbajimadini.
Mchango wa hawa wanawake wachimbaji kwa jamii na taifa ni mkubwa na sote hatuna budi
kuutambua, kutunuku na kuboresha zaidi kwa kutatua changamoto wanazokabiliana nazo
katika uchimbajimadinimigodini.
Kwa msingi huo basi Tanzania WomenMiners Association (TAWOMA) imebunituzo yaMalkiawa
madini ambayo; mosi, itafanikisha utambuzi wa juhudi za wanawake wanaojishugulisha
kwenye mnyororo mzima wa thamani ya madini Tanzania, lakini pili itaibuamiradimbalimbali
ya kuwajengea uwezo wanawake wachimbaji kwenye maeneo yote ya maudhui ya tuzo ya
Malkia wa madini ili kumboresha mwanamke mtanzania anayejihusisha kwenye shughuli za
uchimbajimadini kilamwaka.
Tuzo hizi kwa mara ya kwanza zitatolewa kwenye Kongamano la Miaka 25 ya TAWOMA
litakalofanyika GeitaMjiniMwezi September 2023.
Follow the below link : -